MAREKANI-MAHAKAMA

Mwanajeshi alievujisha siri za Marekani kwa mtandao wa Wikileaks ahukumiwa kifungo cha miaka 35 jela

Mwanajeshi alievujisha siri za Marekani kwa Weakiliks Bradley Manning
Mwanajeshi alievujisha siri za Marekani kwa Weakiliks Bradley Manning

Mahakama moja nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha miaka 35 jela, mwanajeshi wa Marekani, Bradley Manning baada ya kumkuta na hatia ya kuvujisha siri za usalama wa taifa lake kwa mtandao wa wikileaks na kushirikiana na makundi na magaidi. Takriban nyaraka mia saba za siri ya Marekani zinadaiwa kuvujishwa na mwanajeshi huyo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya zaidi ya miezi miwili ya kesi hiyo, hakimu wa kijeshi Denise Lind pia aliamua kutimuliwa katika jeshi la Marekani kwa mwanajeahi huyo kwa kosa la kuliaibisha hususan kuhusu upelelezi na udanganyifu na wizi wa nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia, ambazo alizituma kwenye mtandao wa Wikileaks. Mwendesha mashtaka alikuwa ameomba angalau kifungo cha miaka 60 jela lakini hukumu hiyo imeonekana kuwa ndefu mno dhidi ya  kosa la kuvujisha nyaraka za siri.

Kimya kilitawala ndani ya mahakama wakati hukumu iliposomwa ambapo kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari, manning amesema kuwa yuko tayari kutumikia adhabu aliyopewa na mahakama.

Kwa mujibu wa mtandao unaomuunga mkono mwanajeshi u

huyo, Wakili wa Manning David Coombs amesema atamwandikia barua rais Barack Obama ampunguzie kifungo kijana huyo ama kumuachia huru.

Siri zilizovujishwa na manning kwa mtandao wa wikileaks ni miongoni mwa kesi kubwa zaidi za uvujishaji siri kwenye historia ya Marekani.