Zimbabwe-Mugabe

Rais Robert Mugabe aapishwa kwa muhula mwingine wa saba mbele ya halaiki ya watu wakishiriki pia viongozi mbalimbali kutoka mataifa yas Afrika

Robert Mugabe akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa tena wakati wa siku ya mashujaa Agosti 12, 2013
Robert Mugabe akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa tena wakati wa siku ya mashujaa Agosti 12, 2013 REUTERS/Philimon Bulawayo (

Rais wa Zimbabwe Comrade Robert Gabriel Mugabe hii leo amekula kiapo cha kuitumikia nchi hiyo kwa muhula wa 7 mfululizo katika sherehe zinazofanyika mjini Harare. Maelfu ya raia wapatao elfu 60 wamehudhuria sherehe hizo ambapo pia viongozi mbalimbali wa bara la Afrika wamealikwa.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo zinafanyika baada ya mahakama kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upinzani kupinga matokeo hayo na kumtangaza rais Mugabe kama mshindi halali huku pia viongozi wa MDCT wakiwa hawajaalikwa kwenye sherehe hizo.

Ma rais kadhaa wa bara la Afrika tayari wamewasili jijini Harare kuhudhuria katika sherehe hizo.

Hivi majuzi viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC waliitaka jamii ya kimataifa kuiondolea vikwazo Zimbabwe, baada ya uchaguzi kufanyika katika hali tulivu.

Marekani tayari imetangaza kuindolea vikwazo Zimbabwe pale tu rasi mugabe atakuwa tayari kufanya mageuzi kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wake.

Rais Mugabe anatimiza mwaka wa 33 madarakani na kuwa mmoja kati ya viongozi wa gra la Afrika aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi huku mwenyewe akitamba kutaka kuongoza taifa hilo mpaka atakapofikisha umri wa miaka 100.

Hivi sasa rais Mugabe ana umri wa miaka 89.