SYRIA-UN

Utata waendelea kulikumba tukio la mashambulizi ya bomu za kemikali katika jiji la Damascus nchini Syria

Watu waliowasilishwa na upinzani kama manusura wa tukio la shambulio la bomu zenye kemikali mjini Damascus, Agosti 21, 2013.
Watu waliowasilishwa na upinzani kama manusura wa tukio la shambulio la bomu zenye kemikali mjini Damascus, Agosti 21, 2013.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameeleza kusikitishwa kwake na tukio la mauaji kwa kutumia silaha za kemikali nchini syria lililotokea hivi karibuni. Ban ki Moon ametaka ufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa tukio hilo bila kuchelewa. Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo ameiandikia barua rasmi serikali ya Syria akiita kuwaruhusu wachunguzi wa umoja wa mataifa walioko nchini humo kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo serikali ya Urusi imesema kwamba ni jambo lisilo wezekana kuona mataifa ya Ulaya yanaendelea kutowa wito kwa Umoja wa Mataifa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya serikali ya Syria baada ya kuwepo kwa taarifa za matumizi ya bomu za kemikali

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema kampeni dhidi ya serikali ya Syria, kulitaka baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kijeshi nchini Syria haieleweki na kuongeza kuwa shambulio hilo linalodaiw la bomu za kemikali katika viunga vya jiji la Damascus, linaonyesha wazi kwamba ilikuwa ni uchochezi wa waasi waliotaka kupotosha uchunguzi wenye malengo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema kwa mujibu wa serikali yake shambulio hilo la bomu za kemikali, liliendeshwa na jeshi la Serikali ya rais Assad na kulitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatuwa.

Waziri huyo ametupilia mbali taarifa kwamba shambulio hilo liliendeshwa na waasi wanaopambana na serikali na kuvitishwa mzigo vikosi vya rais Assad.

William Hegue amesema tayari amewasiliana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry pamoja na viongozi wengine hususan wa Uturuki na Qatar, na  kuongeza kuwa anamatumiani ya kuwasiliana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi.

Amesema kwamba wanachokifanya cha dharura kwanza ni kuhakikisha timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa inaruhusiwa kufanya uchunguzi kwani amesisitiza hadi sasa serikali ya rais Assad haijawaruhusu kwenda kufanya uchunguzi.