Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC huku shinikizo la kuchukunguzwa kama silaha za kemikali zimetumika nchini Syria likizidi

Sauti 20:42
Wanajeshi wa Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa kwenye doria katika Mji wa Goma kukabiliana na Kundi la Waasi la M23
Wanajeshi wa Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa kwenye doria katika Mji wa Goma kukabiliana na Kundi la Waasi la M23 Reuters

Kikosi cha Umoja wa Mataifa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimeamua kuingilia kati mapigano mapya yaliyozuka Mashariki mwa DRC kwa kutoa usaidizi kwa Jeshi la FARDC linalopambana na Kundi la Waasi la M23, Hali ya wasiwasi imeendelea kutamalaki nchini Misri kipindi hiki Kiongozi wa zamani wa Taifa hilo Hosni Mubarak akiachiwa kwa masharti huku Viongozi wa Chama Cha Muslim Brotherhood wakiendelea kushikiliwa na Mataifa ya Magharibi wamezidisha shinikizo kwa Serikali ya Syria kukubalia kufanyika kwa uchunguzi kubaini iwapo shambulizi lililotekelezwa kwenye viunga vya Damascus kama lilitumia silaha za kemikali!!