Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Kundi la Waasi la M23 lataka mazungumzo na Serikali ya DRC huku Mkutano wa G20 ukishindwa kuafikiana juu ya kuivamia kijeshi Syria

Imechapishwa:

Kundi la Waasi la M23 limepokea kwa mikono miwili ushauri uliotolewa na Viongozi wa Nchi wanachama kumi na moja za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR ambao wametaka wao na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kurejea kwenye meza ya mazungumzo kusaka suluhu ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Taifa hilo na Mkutano wa Viongozi wa Mataifa Ishirini Tajiri Duniani maarufu kama G20 wametamatisha Mkutano wao nchini Urusi huku wakishindwa kuafikiana juu ya pendekezo la Marekani la kutaka kuivamia kijeshi nchi ya Syria!!

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye Mkutano wa ICGLR huko Kampala
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye Mkutano wa ICGLR huko Kampala
Vipindi vingine