INDIA

Mahakama kuu nchini India yawakuta na hatua watuhumiwa 4 wa ubakaji

Baadhi ya wananchi wa India wakiandamana kushinikiza haki kutendeka dhidi ya watuhumiwa wa ubakaji
Baadhi ya wananchi wa India wakiandamana kushinikiza haki kutendeka dhidi ya watuhumiwa wa ubakaji Reuters

Majaji wa mahakama kuu nchini India hii leo imewakuta na hatia watuhumiwa wa 4 wa ubakaji kwenye kesi ambayo hukumu yake inasubiriwa kwa hamu kubwa na maelfu ya wananchi wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na maelfu ya wananchi wa India tayari imeanza kuvuta hisia za wanafamilia wa ndugu waliopoteza mtoto wao kwa kubakwa wakishinikiza watuhumiwa hao kupewa adhabu ya kifo.

Watuhumiwa hao wanne watarajiwa kupanda kizimbani muda wowote kuanzai sasa kusikiliza hukumu yao ambayo kwa sehemu kubwa majaji wanatarajia kuwahukumu kunyongwa kutokana na makosa waliyotenda.

Watuhumiwa hao, Mukesh Singh, Akshay Thakur, Pawan Gupta na Vinay Sharma wamekana mashtaka yanayowakabili.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutekeleza unyama huo mwezi December mwaka jana majira ya jioni kwa kuingia kwenye basi na kumteka msichana huyo pamoja na mpenzi wake na kisha kuanza kumbaka na kumuingizia chupa sehemu zake za siri hadi kufa.

Mtuhumiwa mwingine ambaye alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati akitekeleza shambulio hilo yeye amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwenye gereza la mafunzo mjini New delhi.

Mtuhumiwa mwingine ambaye ni dereva wa basi ambalo watuhumiwa hao walilitumia alikutwa amejinyonga kwenye chumba chake cha magereza mwezi March mwaka huu.

Serikali ya India imekuwa ikikosolewa kwa sehemu kubwa na jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za wanawake kwakushindwa kusimamia sheria ambazo imezitunga dhidi ya ukatili wa wanawake huku vitendo vya ubakaji vikiongezeka.