SYRIA-MAREKANI-URUSI

Waasi wa jeshi huru la Syria wapinga mapendekezi ya nchi ya Urusi kuhusu silaha za kemikali nchini humo

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kulia) akiwa na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov (kushoto)Ngoại giao Hoa Kỳ ở Washington ngày 09/08/2013.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kulia) akiwa na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov (kushoto)Ngoại giao Hoa Kỳ ở Washington ngày 09/08/2013. REUTERS/Gary Cameron

Waasi wa jeshi huru la Syria wametangaza kutoutambua mpango wa Serikali ya Urusi kuhusu utawala wa rais Assad kuruhusu silaha zake za kemikali kuteketezwa na kuwa chini ya uangalizi wa jumuiya ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na kundi hilo kupitia njia ya mtandao wa youtube imesema kuwa kamwe hawautambua mpango uliopendekezwa na serikali ya Urusi, kwa kile inachodai kuwa unalenga kuisaidia Serikali ya Syria.

Kamanda wa waasi hao wa Syria amesema kuwa mpango wa Syria unalenga kutoa nafasi zaidi kwa utawala wa rais Bashar al-Assad kupata mwanya wa kuzificha silaha zake za kemikali.

Waasi hao pia wamekosoa hatua ya Marekani kusitisha mpango wao wa kuivamia kijeshi nchi ya Syria kwa madai kuwa kufanya hivyo kunawafanya wanajeshi wa Serikali waendelee kupata nguvu zaidi ya kuwashambulia na kuchukua maeneo zaidi.

Tayari Serikali ya Urusi imewasilisha mapendekezo yake manne kwa Serikali ya Marekani kuhusu hatua za kuchukua ili kuhakikisha utawala wa Syria unasalimisha silaha zake za kemikali kwa wakati.

Bila ya kuzitaja hatua ambazo zitachukuliwa, waziri wa mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov anasema kuwa mapendekezo hayo manne yatakuwa yamanufaa kwa wahusika wote wa mgogoro wa Syria na yatarahisisha zoezi la kukusanya silaha hizo.

Juma hili rais wa Marekani, Barack Obama alisitisha mpango wake wa kuitisha kura kwenye bunge kutaka waamue iwapo waidhinishe mpango wa kuishambulia kijeshi nchi ya Syria, mkakati ambao ulipingwa vikali na Serikali ya Urusi.