URUSI-SYRIA-MAREKANI-UINGEREZA

Serikali ya Urusi yatowa tahadhari kwa mataifa ya Ulaya juu ya mpango wa Kuishambulia Syria

Serikali ya Urusi imetahadharisha kuhusu rasimu ya azimio la baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayo tishia serikali ya Syria na ambao hauheshimu makubaliano ya Giniva, wakati Ufaransa, Uingereza na Marekani vikijiandaa kuwasilisha muswa huo tata.

Waziri wa ammbo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa ammbo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Urusi Sergei lavrov amewaambia wanandishi wa habari kwamba anaimani kuwa matamshi yanayotolewa na mataifa ya Ulaya kuhusu Syria, Marekani ambayo ni mshirika itajizuia kuhusu yaliofikwa ikiwa kweli ni mshirika aliey makini.

Urusi na Marekani zilifikia makubaliano mwishoni mwa muma lililopita jijini Giniva Uswisi kuhusu mpango wa kuharibu silaha za Kemikali za serikali ya Damascus.

Waziri huyo wa mambo ya ndani ameendelea kuwa hakuna kitisho chochote cha kutafuta sababu ya kuishambulia Syria kijeshi na hii ni njai ambayo itaharibu mipango yote ya kutafuta suluhu kwa matatizo yalipo kwa sasa nchini Syria hasa maandalizi ya mkutano wa Giniva 2, mkutano wa kimataifa ambao Jumuiya ya kimataifa unaandaa kupanga ili kumaliza machafuko nchini Syria.

Waziri Lavrov ameyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje wa Misri Nabil Fahmy
Kiongozi huyo wa Urusi amesdema ni lazima kuelewa kwamba kama wanataka kushughulikia suala la uharibifu wa silaha za kemikali nchini Syria, basi Makubaliano ya Urusi na Marekani yanatowa njia ya kitaalamu na ilio wazi

Amesisitiza kwamba makubaliano yaliofikiwa siku ya Jumamosi baina yake na waziri wa mambo ya nje wa Marekani hayakutowa azimio litakalotumika kwa mara ya kwanza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuvunjwa silaha za kemikali nchini Syria na hayakutaja kutaja ya matumizi ya sura ya 7 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambayo inatowa mamlaka ya matumizi ya nguvu.