SYRIA-MAREKANI-URUSI

Marekani na washirika wake waendeleza shinikizo zaidi juu ya uwepo wa azimio kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria

Marekani na washirika wake waendelea kusisitza juu ya uwepo wa azimio kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya bomu za sumu nchini Syria na kuitishia serikali ya rais Assad kuhusu madhara yatayoweza kujitokeza kama itashindwa kuheshimu majukumu yake. Serikali za Washington na Paris zinazingatia ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya bomu za kemikali iliotolewa jana Jumatatu kwamba kuna ushahidi mkubwa wa matumizi ya bomu aina ya sarin Agosti, 21, na kuiweka hatiani serikali ya huko Damascus.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na wa Urusi Sergei Lavrov
Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na wa Urusi Sergei Lavrov Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye serikali yake inapinga vikali uwepo wa azimio lolote kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, anakutana kwa mazungumzo na mwenziwe wa Ufaransa Laurent Fabious.

Wakati huo huo rais wa Ufansa Francois Hollande anakutana na waziri wa mambo ya nje wa Qatar Khaled Attiyah ambapo watajadili kuhusu mzozo wa Syria

Ikulu ya Marekani imesema jana Jumatatu kuwa ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya matumizi ya bomu zenye kemikali nchini Syria mwezi uliopita inaonyesha kuwa serikali ya Bashar al-Assad inahusika.

Msemaji wa Ikulu ya White House Jay Carney amesema ripoti hii, inaonyesha kwamba silaha zenye kemikali zilitumiwa na ambazo huwezi kuzitumia bila kuwa na vifaa maalum na ambavyo serikali pekee ndiyo inavyo vimiliki

Wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao walipewa jukumu la kuendesha uchunguzi kuhusu matumuzi ya silaha zenye kamikali katika shambulio la Agosti 21 nchini Syria ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 1400, ripoti ambayo ilitolewa jana inaonyesha ushahidi wa kutosha wa uwepo wa matumizi hayo.

Katika Ukurasa wa kwanza wa ripoti, hiyo ilikanbidhiwa kwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon na mkaguzi mkuu Sellström Aake inaonyesha kuwa silaha za kemikali zilitumika kwa kiwango kikubwa katika mgogoro unaendelea nchini Syria na ambapo waathirika ni raia, lakini pia watot