URUSI-UN

Serikali ya Urusi yaituhumu ripoti ya watalaamu wa Umoja wa Mataifa, na kusema kuwa imeegemea upande mmoja

Serikali ya Urusi imewatuhumu wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliofanya uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, kuegemea upande mmoja. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Serguei Riabkov amesema wanasikitishwa na mwenendo wa wataalamu hao ambao hawakutilia maanani taarifa ambazo tumekuwa tukizitowa mara kw amara.

Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia huyo wa Urusi ambaye amewasili jijini Dmascus jana, amesema kwamba wataalamu hao waliochapisha ripoti yao walichukulia pekee tukio la Damascus la Agosti 21 bila kutilia maanani matukio mengine matatu.

Naibu waziri huyo amesema kuna taarifa ambazo walipokea kutoka kwa serikali ya Urusi inayo watuhumu waasi katika sakata hilo la matumizi ya silaha zenye kemikali.

Serikli ya Urusi imeanza kufanya uchunguzi kuhusu taarifa hizo, ambapo kwa sasa hawajatmatisha uchunguzi huo na watatilia maanani taarifa hiyo iliowahusisha waasi wa Syria katika shambulio la Agosti 21.

Wataalamu wa Urusi wanafanya uchunguzi wa kina ambapo naibu waziri wa mambo ya nje Riabkov amesema ushuhuda huo utasaidia kutowa ushahidi juu ya waasi kuhusika katika matumizi ya silaha za Kemikali.