SUDANI-UN

Umoja wa Mataifa wamtaka rais wa Sudan Omar Al Bashir kushirikiana na mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC

Rais wa  Sudani Omar Hassan Al Bashir
Rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir un.org

Umoja wa Mataifa umependekeza kwa  Rais wa Sudan Omar al-Bashir kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ya (ICC), na kuongeza kuwa, Marekani yenyewe ndio itayo amuwa kumpa visa au la ya kushiriki katika mkutano mkuu wa Umoja huo mwishoni mwa mwezi huu jijini New York.l

Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kupitia msemaji wake Martin Nesirky, amemtaka Rais wa Sudan, Omar al Bashir kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kivita,

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo hali ya mkanganyiko baada ya Kiongozi huyo wa Sudani kuomba Visa kwa Marekani, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema  hili ni jukumu la Marekani yenyewe kuamua juu ya suala la visa kwa mujibu wa sheria husika za kimataifa.

Marekani haiungi mkono kitendo cha Bashir kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa, lakini imekataa kueleza kama itamzuia Kiongozi huyo kuingia nchini Marekani au la.

Ban Ki Moon amemtaka Rais Bashir kutoa ushirikiano kwa mahakama ya ICC.mahakama hiyo ilitoa Waranti ya kukamatwa kwake mnamo mwezi March mwaka 2009 na Julai mwaka 2010, na kuwa anakabiliwa na mashtaka 10 ya uhalifu wa kivita, yakiwemo mauaji ya halaiki na ukiukwaji wa haki za binaadam wakati wa mgogoro wa Darfur.

Kwa mujibu wa serikali ya Sudan, Rais Bashir anataka kutembelea kwenye baraza la Umoja wa Mataifa na sio nchini  Marekani. Serikali ya Marekani inawajibika chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kutotia pengamizi la kutowa viza kwa wanachama wa Umoja huo.

Kulingana na Mkataba wa mwaka1947 kati ya Umoja wa Mataifa na Marekani, mwenyeji wa shirika la kimataifa unasema kwamba Marekani haipaswi kulazimisha vikwazo kwa wawakilishi wa nchi wanachama ambao wanataka kutembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.