MALI-SHEREHE

Wageni waalikwa kutoka Jumuiya ya Kimataifa wameanza kuwasili jijini Bamako kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais IBK

ibrahim Boubacar Keïta wakati akila kiapo Septemba 4
ibrahim Boubacar Keïta wakati akila kiapo Septemba 4 REUTERS/Joe Penney

Wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wameanza kuwasili jijini Bamako kuhudhuria sherehe rasmi za kuapishwa kwa rais wa Mali Ibrahim Bubakar Keita ambazo zimepangwa kufanyika kesho siku ya alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Takriban ma rais 26 na serikali wanasubiriwa kwenye sherehe hizo wakiwemo mrais wa Ufaransa Francois Hollande, Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire, Idris Deby Itno wa Tchad pamoja na mfalme wa Moroco Mohamed VI.

Bubakar Keita alishinda uchaguzi wa Agosti 11 na tayari amekula kiapo Septemba 4 ili kuheshimu katiba ya taifa hilo ambapo hapakuwepo na sherehe yoyote. Alhamisi Septemba 19 ndipo kutakuwa na sherehe kabambe kwenye uwanja wa michezo wa March 26 wenye uwezo wa kupokea watu elfu hamsini na tano, huku viongozi kutoka katika mataifa mbalimbali wakihudhuria.

Kulingana na kalenda iliotolewa na ikulu ya rais nchini Mali, rais Ouattara ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS, pamoja na mfalme wa Moroco Mohamed VI, rais wa Idris Deby Itno na Francois Hollande wanatahutubia katika sherehe hizo.

Hii ikiwa ni kuonyesha umuhimu wa mataifa hayo katika kuushughulikia mzozo wa Mali. Ma rais Hollande, Idris Deby, Ouattara wataendesha mkutano wa pamoja na rais Keita alhamisi baada ya sherehe hizo Ikulu ya rais.

Ufransa ndio ilikuwa kwenye mstari wa mbele katika operesheni dhidi ya makundi ya kigaidi yaliokalia eneo la kaskazini mwa Mali katika kipindi cha zaidi ya miezi mitano.

Takriban wanajeshi 4.500 wa Ufaransa wameshiriki katika operesheni iliobatizwa Serval nchini Mali, ambpo Tchad pia iliwatuma wanajeshi wake 2000 waliokuwa bega kwa bega na wafaransa katika kufaanikisha operesheni hiyo.

Miezi minane tangu kumalizika kwa operesheni hiyo, takriban wanajeshi 3200 wa ufaransa bado wapo nchini Mali, ambapo serikali ya Ufaransa imesema wataendelea kupunguza idadi hiyo hatuwa kwa hatuwa hadi mwishoni mwa mwaka huu.