Rais wa Syria Bashar Al Assad atowa ahadi ya kuharibu silaha zake za kemikali kwa kipindi cha mwaka mmoja
Rais wa Syria Bashar al-Assad ameahidi kuharibu silaha zake za kemikali katika kipindi cha mwaka mmoja lakini amesema zoezi hilo linahitaji kitita cha dola za marekani bilioni moja.
Imechapishwa:
Assad ameyasema hayo katika kituo kimoja cha TV cha FoxNews ambacho kimemuonyesha Assad akiwa mwenye kujiamini wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likijadili kuhusu azimio ambalo linaagiza matumizi ya nguvu dhidi ya utawala wake, iwapo hatoheshimu mpango wa kuharibu silaha za kemikali uliofikiwa Septemba 14 kati ya Moscou na Marekani.
Katika hatua nyingine Rais Bashar al Assad ameitaka Marekani kuacha kuitishia syria na badala yake kusikiliza sauti ya wananchi wa syria.
Kwa kipindi cha miaka miwili, takriban watu laki moja na elfu kumi wamepoteza maisha, huku rais wa Syria akithibitisha kwamba nchi yake haipo kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe bali inakabiliana na vita dhidhi ya makundi ya kigaidi yenye kukusanya raia kutoka nchi 80 za kigeni ambapo asilimia 80 na 90 ni wapiganaji wa Alqaeda.
Tangu mwezi March 2011, ma mia ya raia wa Syria na takriban wanajeshi 15.000 wa serikali wameuawa ambapo kwa asilimia kubwa kutokana na mashambulio ya kigaidi
Katika mahojiano haya ya pili katika kituo cha televisheni cha Marekani Rais Assad amesisitiza kuwa shambulio la bomu zenye kemikali lililotokea Agosti 21 karibu na mji wa Damascus ni tukoo la waasi wanajeshi wa serikali yake hawajahusika.
Hayo yanakuja wakati huu Urusi ikidai kuwa ina ushahidi unaoonyesha dhahiri kuwa upande wa upinzani ndiyo ulitumia silaha za kemikali ambapo waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Serguei Lavrov ameendelea kusisitiza, wakati ambapo mataifa ya magharibi na nchi kadhaa za kiarabu zikiilamu serikali ya Assada kuhusika na shambulio hilo.