MALI-SHEREHE

Rais wa Ufaransa Francois Hollande anogesha sherehe za kuapishwa kwa rais wa Mali Brahim Bubakar Keita

Rais wa Mali Ibrahim Bubakar Keita(IBK) amekula kiapo leo kwenye sherehe za hadhara zilizo fanyika kwenye uwanja wa michezo wa jijini Bamako, huku wakihudhiria halaiki ya wananchi wa taifa hilo na marais zaidi ya ishirini kutoka katika mataifa mbalimbali akiwemo rais wa Ufaransa Francois Hollande.

Rais wa Mali IBK
Rais wa Mali IBK
Matangazo ya kibiashara

Akiwahutubia halaiki ya watu na viongozi wa mataifa zaidi ya ishirikini waliokuwepo kwenye sherehe hizo za hadhara za kula kiapo kwa rais Ibrahim Bubakar keita, rais wa Ufaransa Francois Hollande ambaye nchi yake ilwatuma wanajeshi wake nchini Mali kuwaunga mkono wanajeshi wa Mali kupambana na wanamgambo wa kigaidi, amesema, “Tumeshinda vita hivi” kabla ya kuongezeka kwamba “ tunaelekea mwisho kwakuwa ni ushindi, ushindi mkubwa kwa Mali ambao tunasherehekea leo na ufaransa inajisufu sana kuchangia katika ushindi huu.”

Mbali na hutuba ya rais Hollande, rais wa Cote d'Iovire Allasane Ouattara mwenyekiti wa Jumuiya ya kiuchumi ya magharibi mwa Afrika ECOWAS ambaye amepongexa hatuwa hiyo iliofikiwa nchini Mali.

Rais wa Tchad Idriss Deby Itno ambaye pia wanajeshi wake wameshirika katika operesheni ya kuwafurusha wanamgambo wa makundi ya kigaidi waliokuwa wakikalia eneo la kaskazini mwa taifa hilo amepongeza pia wananchi wa Mali kwa kufanya maamuzi mazuri mazuri hasa katika kuendesha uchaguzi katika hali tulivu.

Akiwahutubia wangeni wa heshma, rais Keita amewasifu ma rais wote walioshiriki katika sherehe hizo huku akionyesha umuhimu wa ushirikiano na kutetea kauli mbiu yake wakati wa kampeni ya uchaguzi "Mali kwanza"

Rais IBK ameahidi kuendeleza harakati za kupiga vita ulaji rushwa, kudumisha utawala bora