MAREKANI-UN

Marekani yataka Umoja wa Mataifa uchukue hatua dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali

Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 20minutes

Serikali ya Marekani imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuja na azimio la pamoja kuhusiana na matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria kwenye mkutano wa umoja huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo mjini NewYork.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa mgogoro wa syria hivi sasa umefikia katika hatua ya mvutano na kinachotakiwa ni umoja wa mataifa kupitia baraza lake la usalama kutekeleza kazi zake kwa vitendo.

Kerry amesema kuwa muda malumbano umekwisha na kinachotakiwa ni kuhakikisha silaha za kemikali zinaharibiwa huko syria kwa sababu tafsiri ya ripoti ya umoja wa mataifa inaonyesha kuwa serikali ya syria inahusika na matumizi ya silaha hizo.

Kiongozi huyo amesema umoja wa mataifa unawajibika kujiandaa kuchukua hatua kuhusiana na silaha hizo za kemikali ambazo zimesababisha mauaji ya raia wasio na hatia.

Wakati huohuo Rais Iran Hassan Rowhani amesema kuwa yuko tayari kuratibu mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Syria na upinzani ili kumaliza mgogoro huo ambao unaendelea kuiyumbisha jumuiya ya kimataifa.

Rais Iran Hassan Rowhan amesema kuwa nchi yake iko tayari kusuluhisha pande hizo ili amani ipatikane nchini Syria kama njia ya kutekeleza sera ya Iran ya kujenga badala ya kubomoa.

Serikali ya Syria bado inashikilia msimamo wake kuwa haikutumia silaha za kemikali licha ya kukubali kuziharibu ndani ya mwaka mmoja .silaha hizo ambazo inazimiliki