Afghanistan-Mauaji

Polisi 18 wameuawa katika shambulio lililoendeshwa na wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan

Wapiganaji wenye silaha wamefanya shambulio la kushtukiza kwenye kituo cha polisi kwenye mji wa Badakhshan nchini Afghanistan na kuua zaidi ya polisi 18, wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imethibitisha.

Les forces de sécurité afghanes inspectent le véhicule piégé qui a été utilisé dans l'attaque, ce 13 septembre 2013.
Les forces de sécurité afghanes inspectent le véhicule piégé qui a été utilisé dans l'attaque, ce 13 septembre 2013. REUTERS/Mohammad Shoib
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, imesema kuwa polisi hao walishambuliwa wakiwa kwenye msafara wakirejea toka kwenye mji wa Warduj ambako walikuwa wakifanya operesheni ya kuyasaka makundi ya wapoganaji yanayohatarisha usalama kwenye eneo hilo.

Shambulio hilo linatokea wakati huu ambapo polisi nchini humo wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya kuwadhibiti wapiganaji wa kundi la Taliban ambao wamekuwa wakiendesha mashambulizi dhidi yao.

Waziri wa mambo ya ndani nchini humo amepongeza vikosi vya Polisi nchini Afghanistani kwa kufaanikiwa kuwauwa na kuwajeruhi wapiganaji wa makundi ya kigaid katika mji huo wa Warduj.

wapiganaji wa Taliban walijigamba kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika mji huo ulio mbali kidogo na ngome yao kuu ya kusini mwa nchi hiyo ambako waasi wamezidisha hujuma na ambapo sasa wamefaulu kutekeleza mashmbuliz katika maeneo zaidi  ya kaskazini.

Wapiganaji hao wa Talibans waliawauwa wanajeshi 17 mwezi march iliopita baada ya kuwateka katika mji huo wa Warduj ya Badakhshan, moja katika ya mikoa yenye utulivu nchini humo

Juma hili Talibans walitangaza kumuawa kiongozi wa tume ya uchaguzi katika mji wa Kurduz ikiwa ni muda mfupi baada ya kuzinduliwa harakati za kuwania uchaguzi wa kumrithi rais wa sasa Hamid Karzai katika uchaguzi wa mwezi April mwakani.