Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mashahidi wa Kesi inayowakabili Wakenya watatu waanza kutoa ushahidi wao faraghani huku Marekani ikiendelea kushinikiza nguvu zitumike kuteketeza silaha za kemikali zinazomilikiwa na Syria

Sauti 20:36
Naibu Rais wa Kenya William Samoei Arap Ruto akiwa na Mwandishi wa Habari Joshua Arap Sang ambao wanakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya ICC
Naibu Rais wa Kenya William Samoei Arap Ruto akiwa na Mwandishi wa Habari Joshua Arap Sang ambao wanakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya ICC Reuters

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC imeamuru mashahidi wanaotoa ushahidi katika kesi inayowakabili wakenya watatu Rais Uhuru Muigai Kenyatta, Naibu Rais William Samoei Arap Ruto na Mwandishi wa Habari Joshua Arap Sang wataendelea kutoa ushuhuda wao faraghani baada ya kuwepo kwa njama za kuwatambua mashahidi kulikofanywa na mitandao ya kijamii na Marekani inaendelea kusimama kidete kuhakikisha wanaungwa mkono kwenye mkakati wao wa kushinikiza nguvu zitumike kuushinikiza Utawala wa Rais Bashar Al Assad inateketeza silaha za kemikali inazomiliki!!