Uganda yatoa wito wa kuongezwa kwa bajeti kusaidia Kikosi cha AMISOM kinachopambana na Kundi la Al Shabab nchini Somalia

Sauti 09:54
Wanajeshi wa Kikosi cha AMISOM wakiwa kwenye doria zao nchini Somalia kudhibiti hali ya usalama
Wanajeshi wa Kikosi cha AMISOM wakiwa kwenye doria zao nchini Somalia kudhibiti hali ya usalama AFP/AU-UN/Stuart Price

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amejitokeza na kutoa wito wa kuongezwa kwa msaada zaidi ili kuhakikisha Kikosi cha Umoja wa Afrika Kinacholinda Amani nchini Somalia AMISOM kinakuwa na uwezo wa kutosha kukabiliana na Kundi la Wanamgambo la Al Shabab. Uganda imesema kumekuwa na kitisho kikubwa kutoka kwa Al Shabab na hivyo lazima juhudi ziongezwe ili kuhakikisha Kundi hilo linatokomezwa kabisa!!