BANGLADESH

Baraza la mawaziri nchini Bangladesh lajiuzulu kupisha Serikali mpya ya kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu

Waziri mkuu wa Bangladesh, Sheihk Hasina
Waziri mkuu wa Bangladesh, Sheihk Hasina Reuters

Mawaziri nchini Bangladesh hii leo wamewasilisha barua za kujiuzulu kwa waziri mkuu Sheihk Hasina kwa lengo la kumpa nafasi ya kutengeneza Serikali ya muungano kuelekea uchaguzi mkuu, hatua ambayo imekataliwa na upinzani ambao wanataka Serikali mpya ya mpito.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya mawaziri kujiuzulu inakuja ikiwa zimetimia siku nne za maandamano ya upinzani nchini humo kushinikiza kujiulu kwa Serikali ya waziri mkuu Hasina kupisha Serikali mpya itakayoandaa uchaguzi mkuu.

Kujiuzulu kwa mawaziri kunakuja kama shinikizo la upinzani ambao wanataka Serikali nzima ya waziri mkuu Hasina ijiuzulu na kupisha utawala mpya kabisa jambo ambalo linaonekana kutofanikiwa kwasasa.

Waziri mkuu Hasina amekiri kupokea barua za mawaziri wake kujiuzulu kumpa nafasi kuunda Serikali ya kitaifa na vyama vingine vya upinzani kuandaa uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo upinzani hautaki.

Upinzani nchini humo unataka baraza lote la mawaziri lijiuzulu pamoja na waziri mkuu Hasina na kisha kupatikane waziri mkuu mpya ambaye ataunda Serikali itakayopelekea kupatikana kwa Serikali ya kitaifa.

Chama kikuu cha upinzani nchini Bangladesh cha BNP kimesema hakitashiriki kwenye Serikali yoyote ambayo itaongozwa na waziri mkuu Hasina, hatua ambayo sasa inaendelea kuweka siasa za nchi hiyo kwenye hali mbaya.

Uchaguzi mkuu nchini humo umepangwa kufanyika mwezi January mwaka 2014, wakati huu ambapo nchi hiyo ikishuhudia maandamano makubwa ya nchi nzima yaliyoitishwa na upinzani kushinikiza kupatikana kwa Serikali mpya ya mpito.