EGYPT-URUSI

Misri na Urusi zaanzisha ushirikiano mpya baada ya zaidi ya miaka 30

Waziri wa mambo ya nje za nje wa Urusi, Sergei Lavrov na mwenzake wa Misri wakati ujumbe wake ulipofanya ziara nchini humo
Waziri wa mambo ya nje za nje wa Urusi, Sergei Lavrov na mwenzake wa Misri wakati ujumbe wake ulipofanya ziara nchini humo Reuters

Serikali nchini Misri imepongeza ziara iliyofanywa na ujumbe wa viongozi wa utawala wa Urusi, ujumbe ulioongozwa na waziri wa mambo ya kigeni, Sergei Lavrov na waziri wa ulinzi Sergei Shoigu ikiwa ni ziara ya kihistoria kuwahi kufanywa na viongozi hao toka mapinduzi ya kujeshi. 

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi ya Misri, Jenerali, Abdel Fattah al-Sisi akiongea na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya viongozi hao, amesema nchi yake imefurahishwa na namna ambavyo mazungumzoyao yamekwenda na kukubaliana kuongeza ushirikiano hasa kwenye masuala ya usalama.

Licha ya Ujumbe wa Misri kuondoka nchini humo bila ya kutangaza makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa kati ya nchi hizo mbili, wachambuzi wa mambo wanasema kuwa huenda mataifa hayo yakawa yamekubaliana kuhusu kuuziana vifaa vya kijeshi.

Nchi ya Urusi ilikuwa mshirika wa karibu wa utawala wa Misri wakati wa muungano wa Kisoviet lakini uhusiano huo ulivunjika baada ya kuingia madarakani kwa rais Anwar Saadat.

Ziara ya mawaziri wa Urusi nchini Misri inafanyika wakati huu ambapo ushirikiano kati ya utawala wa Misri na Marekani ukiendelea kuzorota kufuatia hatua ya Marekani kutangaza kusitisha msada wake kijeshi kwa jeshi la nchi hiyo kufuatia kuendelea kuuawa kwa waandamanaji.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa ziara ya Lavrov na waziri wa mambo ya ndani nchini Misri, ililenga kutafuta uungwaji mkono na utawala wa Misri, wakati huu ikijaribu kurejesha uhusiano uliokuwa umedorora kwa zaidi ya miaka 30.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Nabil Fahmy amekanusha taarifa kuwa nchi yao inampango wa kufanyia mabadiliko sera yake ya mambo ya nje na kwamba inataka kuhamishia uhusiano wake na nchi ya Urusi, badala yake akasema kuwa Urusi ni rafiki wa kweli hasa wakati huu nchi hiyo iko kwenye mzozo.