Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Dunia yaendelea kumuenzi Mandela, Kusainiwa kwa makubaliano ya amani baina na M23 na serikali ya Kinshasa, Miaka 50 ya uhuru wa Kenya na Oparesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Sauti 20:37
REUTERS/Benoit Tessier

Katika makala ya Mtazamo Wako kwa Yaliyojiri Wiki hii tutatazama maombolezo ya Rais wa kwanza mweusi wa nchini Afrika Kusini Nelson Mandela ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho jumapili, pia tutatazama kuhusu kusainiwa kwa makubaliano ya amani baina ya serikali ya Kinsaha na kundi la M23, hatuyaweka kando maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya toka ilipoachiwa na wakoloni wa Kiingereza, mwisho kabisa tutaangazia oparesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji inayofanyw ana majeshi ya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.