MADAGASCAR

Wananchi wa Madagascar hii leo wanapiga kuchagua rais mpya kwenye uchaguzi wa duru ya pili

Robinson Jean-Louis mgombea urais kwa tiketi ya chama cha upinzani nchini Madagascar
Robinson Jean-Louis mgombea urais kwa tiketi ya chama cha upinzani nchini Madagascar Reuters

Wananchi wa Madagascar hii leo wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa urais na wabunge kwenye duru la pili la uchaguzi huo, uchaguzi unaolenga kumaliza mzozo wa kisiasa uliodumu kwa miongo kadhaa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa visiwa hivyo wanapiga kura kumaliza mtafuruku wa kisiasa uliozuka nchini humo toka kuingia madarakani kwa rais Andry Rajoelina mwaka 2009 kwa mapinduzi, hali iliyofanya wafadhili kusitisha misaada yao kwenye nchi hiyo.

Rais Rajoelina aliingia madarakani kwa kumpindua mpinzani wake wa karibu, Marc Ravalomanana ambaye amezuiliwa kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu yeye pamoja na Rajoelina kufuatia shinikizo toka jumuiya ya kimataifa.

Kwenye uchaguzi wa awali haukuweza kutoa mshindi wa jumla na badala yake wagombea wawili djio waliolazimika kupitishwa kuwania kjiti hicho kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo ambao unafanyika tena hii leo.

Kwenye kinyang'anyiro cha safari hii wagombea, Robinson Jean Louis atapambana na Hery Rajaonarimampianina kiongozi anayeungwa mkono na rais wa sasa Andry Rajoelina.

Katika uchaguzi wa duru ya kwanza Jean Louis alipata asilimia 21.16 ya kura zote na hivyo kuongoza kwenye awamu ya kwanza, kiongozi huyu anaungwa mkono na rais aliyeko uhamishoni, Marc Ravalomanana.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Louis ananafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kutokana na kupata uungwaji mkono mkubwa toka kwa vya vingine vya upinzani nchini humo.