Ufaransa - Mkutano

Rais Hollande kufanya kikao na waandishi wa habari zaidi ya 600 jijini Paris

François Hollande rais wa Ufaransa
François Hollande rais wa Ufaransa REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Ufaransa Francois Hollande, anatarajia kufanya kikao na vyombo vya habari baadae hii leo na ambapo mbali na maswala ya uchumi, maisha binafsi ya rais Hollande yatagusiwa pia katika mkutano huo unaofanyika wakati huu rais huyo akiendelea kupoteza umaharufu. 

Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa ni mara ya tatu rais Hollande kufanya kikao na vyombo vya habari katika muhula wake. Kabla ya waandishi wa habari kupewa nafasi ya kuhoji maswali, rais Hollande atahutubia kwa muda wa takriba dakika ishirini.

Francois Hollande amekuwa gumzo katika vituo mbalimbali vya kitaifa nchini Ufaransa na vya kimataifa ambavyo vimekuwa vikimuhusisha katika kashfa ya uhusiani wa kimapenzi na Julie Gayet msanii wa filamu nchini humo.

Mwishoni mw ajuma lililopita mke wa rais Hollande alilazwa Hospitali kufuatia mshtuko wa moyo baada ya kupata taarifa za mumewe kuwa na mahusinao wa kimapenzi na mwanamke mwingine.

Takriban waandishi wa habari mia sita watashiriki katika kikao hicho, wakiw ani kutoka ndani na nje ya Ufaransa.

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi madarakani nchini Ufaransa kutajwa katika kashfa ya mahusiano ya kimapenzi ya nje ya ndoa.

Hata hivyo maswala ya siasa za ndani na nje, uchumi na maendeleo ya taifa hilo hususan makubaliano ya rais Hollande na ma kampuni nchini humo kwa ajili ya kuongeza nafasi za ajira, kama alivyo ahidi wakati wa hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa raia, ni miongoni mwa yatayo jiri katika mkutano huo.

Kulingana na taasisi zinazo towa maoni za OpinionWay na Ipsos zimeonyesha kwamba rais Rais Hollande amepoteza umaharufu mkubwa.