Jamhuri ya Afrika ya kati-uchaguzi

Catherine Samba-Panza mea wa jiji la Bangui ateuliwa kuwa rais wa kipindi cha mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mea wa sasa wa jiji la Bangui Catherine Samba-Panza ameteuliwa kuwa rais wa kipindi cha mpito nchini jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kuchaguliwa na bunge la kitaifa nchini humo. Catherine Samba alichuana vikali na Désiré Kolingba, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo André Kolingba.

Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati
Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati RFI
Matangazo ya kibiashara

Wabunge nchi jamhuri ya Afrika ya kati hatimaye wamemchaguwa mea wa jiji la Bangui kuwa rais wa taifa hilo baada ya duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika bungeni na ambao ulikuwa unasubiriwa na wengi nchini humo na nje ya taifa hilo.

Licha ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi, Catherine Samba-Panza alimshinda Désiré Kolingba katika awamu ya kwanza kwa kupata kura 64 lakini alikosa kura moja tu ili kumuwezesha kupata uwingi wa kura.

Rais huyo Mpya amechaguliwa kupata kura 75 dhidi ya 53.

Hakuna dosari zozote zilizo ripotiwa, wagombea wote walipewa nafasi ya kujieleza kwa muda wa dakika 8, huku kila mmoja akitowa ahadi lukuki.

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake, Catherine Samba-Panza amewatolea wito wananchi wa taifa hilo kuweka silaha chini, na kumalizza tofauti zao.