SYRIA-Mazungumzo

Serikali ya Urusi yatetea mualiko wa Iran katika mazungumzo ya awamu ya pili ya mjini Geneva Uswisi baina ya wasi na serikali ya Syria

Sergei Lavrov waziri wa mambo ya nje nchini Urusi
Sergei Lavrov waziri wa mambo ya nje nchini Urusi REUTERS/Adrees Latif

Serikali ya Urusi kupitia waziri wake wa mambo ya nje Serguei Lavrov amesema kwamba kutoialika Iran mabayo ni mshirika wa karibu wa Syria kwenye mkutano wa awamu ya pili wa mjini Geneva Uswisi baina ya serikali ya rais Bashar Al Assad na waasi, ni kosa kubwa lisilo samehewa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri lavrov ameyasema hayo wakati akitowa mtazamo wake juu ya kitisho cha waasi kutohudhuria kwenye mkutano huo baada ya serikali ya Iran kupewa mualiko na Umoja wa Mataifa juu ya kuhudhiria kwenye kikao hicho.

Lavrov amesema iwapo kuna mtu haoni umuhimu wa kushirikisha pande zote husika na mzozo huo, basi mtu huyo atakuwa hana nia ya kutaka kutatua mzozo hu kwa njia ya ukweli na haki. Waziri Lavrov amesema kitisho hicho cha kutoshiriki katika mkutano huo ni madeko ya waasi kwa jumui ya ya kimataifa.

Hayo yanajiri wakati rais Bashar al Assad akinena kuwa yupo tayari kushiriki kwenye uchaguzi iwapo wananchi wake watamuhitaji. Aidha kuhusu mkutano wa awamu ya pili wa Geneva, rais Assad amesema kuwa upinzani umeundwa na idara ya ujasusi kutoka mataifa ya Qatar, Saudia Arabia, Marekanina Ufaransa ambayo ameituhumu kuwa mjube wa mataifa ya Qatar na saudia Arabia.

Muungano wa makundi ya waasi nchini Syria, umetishia kutoshiriki kwenye mkutano huo wa awamu ya pili ya Geneva Uswisi iwapo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon hatowanyang'anya mualiko wawakilishi wa serikali ya Syria.

Mbali na muunganno huo wa waasi, serikali ya Saudia Arabia imekashifu vikali hatuwa hiyo ya kuialika serikali ya Iran kuhudhuria katika mkutano huo wa awamu ya pili ya Geneva