Ukraine-Maandamano

Rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch awatolea wito raia wake kutojiunga na makundi ya wachochezi

Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych
Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych Reuters/Mykhailo Markiv/Ukrainian Presidential Press Service

Rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch amewatolea wito wananchi wake kutoshirikiana na wabaguzi wanaochochea machafuko katika mji mkuu wa taifa hilo wa Kiev yaliosababisha vifo vya watu wawili. Emmanuel Makundi na habari zaidi 

Matangazo ya kibiashara

katika taarifa iliotolewa na ikulu ya, rais Viktor Ianoukovitch amebaini maskitiko yake kuhusu vifo vya watu wawili vilivyosababishwa na vurugu zinazo chochewa na wabaguzi na kuwatolea wito wananchi wake kutoshirikiana na wachochezi wanaolenga kuharibu hatuwa zilizofikiwa na serikali yake.

Polisi nchini humo imeendelea kuwasambaratisha waandamanaji waliokusanyika katika barazabara za mji mkuu Kiev kwa kuwavurumishia bomu za kutowa machozi, huku waandamanaji wakijibu kwa kuwarushia mawe na machupa polisi ambao walijizatiti kuzima waandamano hayo.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umeitolea wito serikali ya Ukraine kusitisha machafuko mara moja baada ya kutokea vifo vya watu wawili mjini Kiev.
Mjumbe wa mambo ya nje kwenye Umoja huo Bi Catherine ashton amesema taarifa za kutokea kwa vifo vya wandamanaji zinaskitisha.

Ashton amezitaka pande mbili kutatua mzozo wa kisiasa kwa njia za amani na kwamba matumizi ya nguvu hayawezi kamwe kuleta suluhusu kwa mzozo huo.

Upinzani nchini Ukraine umeapa kuendelea na maamdano hadi kuungusha utawala wa Ianoukovitch, wakati huo huo naye akiapa kung'atuka madarakani.