Misri-Uhuru

Shirika la kimataifa linalo walinda waandishi wa habari lasema Misri imekuwa nchi hatari kwa waandishi baada ya Syria na Iraq

Mwenyekiti wa shirika linalo walinda waandishi wa habari CPJ
Mwenyekiti wa shirika linalo walinda waandishi wa habari CPJ Reuters

Shirika la kimataifa linalo walinda waandishi wa habari CPJ lenye makao yake makuu jijini New York Marekani limesema katika ripoti yake kwamba uhuru wa kujitetea nchini Misri umeshuka kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2013 ambapo ni kiasi kikubwa ambacho hakijawahi kutokea popote pale duniani.

Matangazo ya kibiashara

Takriban waandishi wa habari 6 walipoteza maisha katika mwaka 2013 na hivo kuifanya Misri kuwa nchi hatari sana kwa waandishi wa habari baada ya Syria na Iraq.

Hayo yanajiri wakati Juhudi zikiendelea kufanywa ili kuwaachia huru waandishi wa habari wa aljazeera wanaozuliwa na utawala wa Misri kwa tuhuma za kutangaza habari ambazo serikali ya nchi hiyo imesema hazina ukweli wowote.

Serikali hiyo imeendelea kuziba maskio ya kuwaacha huru waandishi hao wa habari licha ya jumuiya ya kimataifa ikiwemo Marekani kutowa wito kwa serikali ya Misri kuwaachia huru bila masharti waandishi hao.

Hayo yanajiri wakati kituo cha Aljazeera kikifahamisha kuwa kati ya waandishi wa habari 20 wanaozuiliwa nchini Misri 9 pekee ndio wanaofanya kazi na kituo hicho chenye makao yake makuu nchini Qatar.

Uongozi wa kituo hicho umeitaka serikali ya Misri kutupilia mbali tuhuma dhidi ya waandishi hao, lakini pia waandishi wote wa habari wanaozuiliwa jijini Cairo waachiwe huru.

Mbali na tuhuma za kutangaza habari zisizokuwa na ukweli ndani yake, waandishi hao wa habari wanatuhumiwa kuhusika katika kundi la kigaidi.

Juma hili serikali ya Marekani imeitaka Misri kuwaacha huru waandishi hao wa habari wanaozuiliwa pamoja na wasomi wengine walioonyesha msimamo tofauti na serikali, na kwamba kila mtu anayohaki ya kutowa maoni bila kujali itikadi yake.