Jamhuri ya Afrika ya kati-mauaji

Umoja wa Mataifa na Ufaransa wataka wanajeshi waliohusika na mauji dhidi ya mshukiwa wa kundi la seleka wakamatwe na kuadhibiwa

Askari wa jamhuri ya Afrika ya kati akimkanyaga raia mmoja aliyeshukiwa kuwa mpiganaji wa seleka
Askari wa jamhuri ya Afrika ya kati akimkanyaga raia mmoja aliyeshukiwa kuwa mpiganaji wa seleka REUTERS/Siegfried Modola

Umoja wa Mataifa na Ufaransa unataka adhabu ya mfano  itolewe kwa wote  kwa wahusika wa kitendo cha mauaji ya kutisha kilichotekelezwa na wanajeshi wa jamhuri ya Afrika ya kati mchana kweupe dhidi ya mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa mpiganaji wa kundi la Seleka.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema kufuatia kuongeza kwa hali ya machafuko jijini Bangui Umoja wa Mataifa huenda ukaongeza muda wa kuwepo kwa operesheni Sangaris ya vikosi vya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kwa kipindi zaidi cha miezi sita.

Siku ya jumatano wanajeshi wa Afrika ya kati walimvamia mtu mmoja ambaye walishumu kuwa mpiganaji zamani wa kundi la Seleka na kumuuawa kwa mawe mchana mkweupe, huku wananchi wakishangilia.

Ufaransa imelaani vikali kitendo hicho na kuomba adhabu kali itolewe ambayo itakuwa mfano kwa wengine. Rais wa nchi hiyo Catherine Samba Panza ameamuru kufanyika kwa uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo, hatuwa ambayo imeungwa mkono na Ufaransa

Akizungumza na vyombo vya habari, muakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini jamhuri ya Afrika ya kati Bubakar Gaye, amesema tukio la kumuuwa mtu hadharani huku watu wakishangilia, ni tukio baya la kulaaniwa kwa nguvu zote na kuomba uchunguzi uanzishwe mara moja ili wahusika wahukumiwe na vyombo vya sheria.