Syria -msaada

Umoja wa Mataifa wakubaliana na serikali ya Syria juu ya kutowa msaada wa kibinadamu katika mji wa Homs

L'aide humanitaire va permettre de fournir une aide vitale à quelque 2 500 civils bloqués par les combats. Homs, le 27 janvier 2014.
L'aide humanitaire va permettre de fournir une aide vitale à quelque 2 500 civils bloqués par les combats. Homs, le 27 janvier 2014. REUTERS/Yazan Homsy

Utawala wa Syria na Umoja wa Mataifa UN, wamekubaliana kutowa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wa waliokwama katika jijini Homs lililozingirwa na majeshi ya serikali tangu takriban siku mia sita na ambao wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri Wakati machafuko nchini Syria yakielekea katika mwaka wa 4, takriban watu 136.000 wamepoteza maisha huku kukiwa hakuna dalili zozote za kupatikana kwa muafaka licha ya kutarajiwa kufanyika mazungumzo Februari 10 mjini Geneva kati ya waasi na serikali.

Hapo jana waasi walifanya shambulio kubwa katika jela kuu jijini Aleppo na kuwatorosha mamia ya wafungwa, wakati jeshi la Serikali likiendeleza mashambulizi katika jiji la Alepo na tayari watu 250 wamepoteza maisha katika kipindi cha siku 5.

Umoja wa Mataifa UN umethibitisha kuwepo kwa mkataba kati ya gavana wa jiji la Homs Talal Barazi na mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa Yacoub Helou juu ya kuwaondowa raia wasiokuwa na hatia katika mji huo na kuwatolea msaada wa kibinadamu raia ambao watapenda kusalia jijini huo.

Mzungumzo baina ya serikali ya rais Bashar al Assad na waasi yanatarajiwa kuanzishwa tena Februati 10 jijini Geneva ambapo pande zote mbili zinatakiwa kukubaliana juu ya mustakabali wa nchi hiyo