DRCongo - ICC

Mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC yamkuta na hatia kiongozi wa majeshi zamani mashariki mwa DRCongo Bosco Ntaganda

Muendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda akiwa na Eric MacDonald  wa ofisi  muendesha mashtaka
Muendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda akiwa na Eric MacDonald wa ofisi muendesha mashtaka REUTERS/Michael Kooren

Mahakama ya Uhalifu wa kivita ya ICC ambayo ilikutana jana ili kutowa uamuzi iwapo kiongozi wa zamani wa kivita mashariki mwa DRCongo Bosco Ntaganda ana kesi ya kujibu, na kumkuta na hatia ya kuhusika katika mauji ya kikabila kati ya mwaka 2002-2003 pamoja pia na ubakaji wa watoto.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mbele ya mahakama, muendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda amethibitisha kuwa Ntaganda anahusika na mauji ya kivita kufuatia ushuhuda wa binti mmoja alieingizwa jeshini na ambaye alibakwa mara kadhaa na wanajeshi wa Ntaganda wakati akipewa mafunzo.

Ntaganda ambaye alipewa jina la Terminator kufuatia ukatili wake na kutokuwa na huruma ana tuhumiwa pia kutekeleza ubakaji na kufanya watumwa wa ngono wasichana wenye umri wa chini ya miaka 15. Fatou Bensouda ni muendesha mashtaka mkuu wa ICC

Hata hivyo, upande wa utetezi unaendelea kusisitiza kuwa kiongozi huyo wa zamani wa waasi wa UPC hakuwa na maslahi yoyote kutekeleza mauwaji hayo kwa vile yeye sio wa kabila la Walema au walendu. Marc Desailliers Wakili wa Bosco Ntaganda amesema mteja wake sio mzaliwa wa Ituri na hapakuw ana sababu yoyote ya kutekeleza mauaji.

Wanaharati mashariki mwa DRCongo katika mji wa Ituri, wamesema wanaridhishwa na hatuwa hiyo ya kwanza. Ignace Bingi  mwenyekiti wa masharika ya kiraia katika mji wa Ituri amesema anaimani kwamba haki itatendeka

Ntaganda alijisalimisha mwenyewe mbele ya mahakama ya ICC Machi mwaka 2013 baada ya mambo kuwa mabaya kwake baada ya kugeukana na washirika wake na kulazimika kukimbilia kwenye ubalozi wa Marekani jijini Kigali nchini Rwanda kabla ya kupelekwa Hegue.

Ntganda ana kesi ya kujibu dhidi ya Makosa ya kivita yaliotekelezwa na vikosi vya kundi la FPLC ambavyo Ntaganda alikuwa kiongozi.