Syria-mazungumzo

Upinzani nchini Syria waonya kuwa hautorejea kwenye mazungumzo iwapo hakuna hatuwa itayofikiwa mjini Geneva

Msemaji wa upinzani wa waasi nchini Syria Louay Safi
Msemaji wa upinzani wa waasi nchini Syria Louay Safi

Wajumbe wa upinzani nchini Syria wanaoshiriki katika mazungumzo ya Geneva wameonya kuwa hawatarejea tena katika mazungumzo kama hakutakuwa na hatua itakayopigwa katika mazungumzo yanayoendelea sasa. Hapo jana mpatanishi Brahimi alikutana na kila upande kwa wati wake kabla ya kukutana na pande zote mbili kwa pamoja baadae jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe hao wamesema kuwa kutokuwepo kwa maendeleo katika mazungumzo hayo ni sawa na kupoteza muda kauli ambayo wamaeitoa mbele ya mjumbe wa usuluhishi wa umoja wa mataifa na nchi za kiarabu Lahkdar Brahimi.

Hayo yanakuja huku pande hizo mbili zikiendea kuvutana na kutupiana lawama kuhusu hatua ya kushambuliwa kwa wafanyakazi wa misaada wa umoja wa mataifa hivi karibuni mjini Homs.

Upinzani kwa upande wake unatupa lawama kwa majeshi ya serikali ya Bashar Al Assad kuwa ndiyo yalifanya mashambulizi. Msemaji wa muungano wa upinzani nchini Syria, Louay Safi amesema hawatoendelea na mazungumzo na serikali iwapo hatuwa muhimu haitofia

Kwa upande wake Serikali ya Syria imesema kuwa iko tayari kwa majadiliano yoyote ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Naibu waziri wa mambo ya nje Faisal Maqdad amesema serikali itaendelea kuonyesha nia yake ya kutaka kupatikana kwa siluhu ya mgogoro unaendelea nchini Syria.