Marekani-sudani Kusini

Serikali ya Marekani yaendelea kusisitiza juu ya kumaliza machafuko nchini Sudani Kusini

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry REUTERS/Brendan Smialowski

Marekani imesema kuwa inaguswa na hali ya mambo nchini Sudan Kusini na itaendelea kusimama kidete ili kuhakikisha mgogoro unaondelea nchini humo unamalizika na raia wasio na hatia kulindwa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa mgogoro lazima ufikie kikomo ili kuepusha mauaji ya halaiki yanayoweza kuikumba nchi hiyo changa duniani kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.

John Kerry ameeleza kuwa Marekani haitaki kuiona nchi hiyo ikitumbukia katika machafuko makubwa na kuirejesha nyuma nchi hiyo na kwamba jitihada zaidi zinahitajika ili kuwasaidia watu Sudan Kusini kujenga mustakabali wa baadaye wa nchi yao.

Hayo yanakuja wakati huu mazungmzo ya amani ya awamu nyingine yenye lengo la kumaliza mgogoro baina ya Serikali ya Rais Salva Kiir na waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais, Riekh Machar yakiendelea  kwa mwendo wa kinyonga nchini Ethiopia.

waasi hao wanatishia kuendelea na mazungumzo iwapo serikali ya Uganda haitoondowa majeshi yake nchini Sudani Kusini na kuwaachia huru wafungwa wanne wanazuiliw akatika jela moja jijini Juba.

Ehiopia ambayo ndio inayo simamia mazungumzo hayo imetowa wito pia kwa nchi zilizo yatuma jaeshi yake nchini Sudani Kusini kuyaondowa majeshi hayo ikihofia kuufanya mzozo huo kuwa wa kikanda.