Isreli-diplomasia

Waziri mkuu wa Israel awatuhumu viongozi wa Umoja wa Ulaya kwa kuwaita wanafiki kwa kushindwa kulaani serikali ya Iran kupeleka silaha jijini Gaza

Benjamin Netanyahu,
Benjamin Netanyahu, REUTERS/Sebastian Scheiner/Pool

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amekemea ukimya wa Jumuiya ya kimataifa juu ya hatuwa ya kukamatwa kwa meli iliokuwa na silaha ambayo ilikuwa inasafirishwa kutoka Iran Kuelekea katika ukanda wa Gaza kupitia bahari nyekundi na ambayo ilikuwa ikiongozwa na Komando raia wa Israeli.

Matangazo ya kibiashara

Netanyahu ameutuhumu hasa Umoja wa Ulaya na mkuu wa sera za nje za Umoja huo Catherine Ashton kwa kile alichotaja unafiki wa Viongozi wa umoja huo kushindwa kuchukuwa hatuwa dhidi ya Iran.

Jumapili iliopita Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton alikuwa nchini Iran katika ziara ya kikazi ambapo alikutana na viongozi wa Iran.

Netanyahu amesema hii inaonyesha namna gani unafiki unaendelea kutawala kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya, kwani hakuna kauli zozote zilizo tolewa za kulaaani kitendo hicho cha Iran kusafirisha silaha katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Netanyahu, silaha hizo aina ya Roketi zilizokuwa zikisafirishwa kwenye meli, zingeliweza kuigusa miji ya Tel Aviv, Jerusalam na kando ya mji wa Haifa kaskazini mwa Israeli.

Roketi ambazo hurushwa na makundi ya wapiganaji wa palestina kutoka katika ukanda wa Gaza huishia katika eneo la Ashkelon na kaskazini mwa kaskazini mwa Neguev.

Waziri mkuu Netanyahu na waziri wake wa Ulinzi Moshe Yaalon wameonyesha silaha hizo zilizokuwa zikisafirishwa kutoka nchini Iran kuelekea katika ukanda wa Gaza.

Jeshi na waziri wa Ulinzi wameonyesha silaha hizo walitarajia kusikia kauli za kulaani serikali ya Iran kutoka Jumuiya ya kimataifa kuunga mkono makundi ya kigaidi na mpango wake wa Nyklia.