Syria-uasi

Waasi wa Syria waomba silaha za kisasa ili kukabiliana na vikosi vya serikali ya rais Assad

Upinzani nchini Syria umetowa wito kwa viongozi wa Jumuiya ya nchi za kiarabu wanaokutana kuhakikisha wanapata silaha za kisasa ili kupambana na majeshi ya serikali ya rais Bashar Al Assad, wakati huu Serikali ya Saudia Arabia ikitowa lamawa kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwatupilia waasi katika kipindi hiki kigumu ambapo vita vimechacha nchini Syria.

Viongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu
Viongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kikao cha Jumuiya ya nchi za kiarabu jijini Koweit, kiongozi wa waasi wa Syria Ahmad Jarba amesema wanachokiomba sio kutangaza vita na serikali ya syria bali ni kuishinikiza Jumuiya ya Kimataifa kutowa silaha za kisasa kwa wapigaji wa jeshi huru la Syria.

Wapiganaji hao wa syria licha ya kupiga hatuwa chache katika uwanja wa mapambano kwenye maeneo ya kaskazini magharibi mwa Syria, hawana uwezo wa kupata ushindi wa kutosha mbele ya vikosi vya rais Bashar Al Assad vilivyo jizatiti vya kutosha wakati huu machafuko nchini humo yakiingia katika mwaka wake wa nne.

Saudia Arabia ambayo imekuwa ikiwafadhili waasi wa Syria kupitia mwanamfalme Salmane Ben Abdel Aziz imesema inafa kuwaunga mkono waasi wa Syria ili kuleta mabadiliko nchini Syria kupitia nguvu za kijeshi.

Duru za waasi zimearifu kuwa Marekani inatumia kura ya turufu juu ya swala la kuwapa silaha za kisasa na zenye uwezo mkubwa waasi kwa hofu ya silaha hizo kuanguka mikononi mwa magaidi.

Mpatanishi katika mzozo huo Lakhtar Brahimi amesema msimamo wa Umoja wa Mataifa, ni kwamba hakuna suluhu yoyote kupitia njia za kijeshi na kutowa wito wa kusitishwa kwa harakati za utowaji silaha kwa pande zote mbili.