Chanjo za kupambana na Covid 19 zapendekezwa kutumiwa nchini Tanzania

Sauti 09:21
Chanjo aina ya  AstraZeneca
Chanjo aina ya AstraZeneca LENNART PREISS AFP/File

Kamati maalumu ya Covid 19 nchini Tanzania, imependekeza kwa Serikali ya nchi hiyo kujiunga katika mpango wa dunia wa usambazaji chanjo, Covax, pamoja na kutangaza tahadhari kama mataifa mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwemo kuchapisha takwimu, kufanya vipimo na kuruhusu chanjo.