Madhara ya kutoweka kwa misitu na mabadiliko ya tabia nchi

Sauti 10:09
Msitu wa Mau nchini Kenya
Msitu wa Mau nchini Kenya © AFP/Roberto SCHMIDT

Misitu ni uhai, kama ilivyo kwa maji na viumbe hai wengine katika mazingira yetu. Wataalamu wanasema sehemu kubwa ya athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazoshuhudiwa sasa duniani, zimechangiwa na kutoweka kwa misitu kunakotokana na shughuli za binadamu.Nchini Kenya, mamlaka kwenye taifa hilo zinapanga angalau ifikapo mwaka 2022, taifa hilo liwe na ongezeko la kiwango cha asilimia 10 ya misitu, kutoka asilimia 7.2 ya sasa, ambapo itahitaji kupanda miti bilioni 1 na laki 8.