Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Watanzania waomboleza kifo cha rais wao, Bobi wine akamatwa Uganda, watu 30 wauawa DRC

Sauti 20:11
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Hassan akiwa na rais John Magufuli, Julai 24 2019 jijini Dar es Salaam.
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Hassan akiwa na rais John Magufuli, Julai 24 2019 jijini Dar es Salaam. AFP - ERICKY BONIPHACE

Ni wiki ambayo raia watanzania, wanaomboleza kifo cha rais wao Joseph Magufuli ambaye alikuwa hajaonekana hadharani  kwa zaidi ya wiki mbili baada ya kusambaa kwa uvumi kuwa alikuwa anaumwa maradhi ya moyo kwa mujibu wa tangazo la serikali, nchi za Jumuia ya afrika mashariki zaomboleza pamoja na Tanzania, huko Uganda kiongozi wa upinzani alikamatwa wakati tume ya Monusco huko DRC juma hili iliahidi kuimarisha usalama mashariki mwa nchi hiyo, kimataifa tumeangazia makataa ya Nchini Ufaransa kwa muda wa wiki 4