Usalama waendelea kuzorota DRC, Kenya kufunga kambi za Dadaab na Kakuma mwaka ujao

Sauti 20:03
Rais wa DRC Félix Tsheskedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na wanahabari Jijini Paris. Aprili 27 2021
Rais wa DRC Félix Tsheskedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na wanahabari Jijini Paris. Aprili 27 2021 AP - Thibault Camus

Miongoni mwa habari kuu za dunia tulizokukusanyia katika makala hii kwa juma hili utasikia kauli ya rais wa DRC Felix Tshisekedi akiomba msaada wa Ufaransa kupambana dhidi ya waasi wa ADF mashariki mwa nchi yake, lakini pia afisa wa polisi Eric Saddam akishuhudia kuhusika na mauaji ya dereva wa mwanaharakati Floribert Chebeya, Kenya kufunga kambi 2 za wakimbizi: Dadaab na Kakuma mwaka ujao, machafuko ya nchini Chad, na kasi ya maambukizi ya Corona huko India.