Muziki Ijumaa

Makala ambayo inakupa nafasi ya kujua masuala mbalimbali ya Muziki na Burudani. Ndani ya makala haya utapata taarifa za wanamuziki, historia zao na bila kusahau mahojiano na wanamuziki mbalimbali. Hii ni fursa ya pekee kwa wasikilizaji kujiliwaza baada ya kazi za juma zima kupitia burudani ya muziki. Makala ya muziki ijumaa pia itakuwezesha kufahamu wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujua wanafanya nini.

Makala ya Muziki Ijumaa inakujia kila Ijumaa saa mbili na nusu asubuhi na marudio yake saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo hiyo. Huo ndiyo muda wako muafaka wa kuweza kuburudika kupitia burudani ya Muziki sambamba na kufahamu yale ambayo yanafanywa na wanamuziki duniani kote.

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10