Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Nyumba ya Sanaa Muziki wa kizazi kipya unavyotia fora nchini Tanzania Makala ya Nyumba ya Sanaa ya juma hili, inamwangazia msanii Steven Charles almaarufu Samertz ni mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, sasa amegeukia uimbaji wa muziki huo, Je nini kimetokea kiasi cha kuanza kuimba? ungana na Steven Mumbi akizungumza na Msanii huyo katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.27/05/2023 20:04
-
Nyumba ya Sanaa Maendeleo ya muziki wa Hip Hop mjini Mombasa pwani ya Kenya na Afrika Mashariki Makala hii imejikita katika Mji wa Mombasa pwani ya Kenya kuangazia maendeleo ya muziki wa HipHop na msanii Fikra Teule ambaye katika siku za hivi karibuni aliitoa video yake mpya na sauti inayofahamika kwa jina la SEMA YOTE akiwa amemshirikisha msanii mpya katika tasnia ya muziki anayefahamika kwa jina la Victoria Gichora, ambapo uzinduzi rasmi wa video yake ulifanyika katika kituo cha utamaduni wa Ufaransa Alliance Francaise ya Mombasa na aliwashirikisha wasanii wenzake wa Hip Hop Ohms Law Montana, Azma Mponda na Mwimbaji Babs kutoka Tanzania.Fikra Teule alizitembelea studio zetu maridadi hapa RFI Kiswahili na kuhojiwa na mwandishi wetu mwandamizi Reuben Lukumbuka..20/05/2023 20:01
-
Nyumba ya Sanaa Nyimbo za Injili zakumbwa na mabadiliko ya kiteknolojia Afrika mashariki Mabadiliko ya Sanaa ya uimbaji yamewafikia waimbaji wa nyimbo za Injili, sasa wanafanya Sanaa hiyo kwa kuendana na hali ya mabadiliko ya kiteknolojia kwenye sanaa ya muziki wa kisasa. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na muimbaji wa nyimbo za Injili Goodluck Gozbert.13/05/2023 20:03
-
Nyumba ya Sanaa Sanaa ya uchoraji visiwani Zanzibar Uchoraji ni Sanaa ya Urithi, kutoka Mji Mkongwe visiwani Zanzibar urithi wa sanaa hiyo umetamalaki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia sanaa hiyo.06/05/2023 20:06
-
Nyumba ya Sanaa Maendeleo ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya eneo la mashariki mwa DRC Muziki ni sanaa inachipuka kwa kasi eneo la mashariki mwa DRC, wasanii wanafanya sanaa inakubalika miongoni mwa jamii inayosikiliza lugha adhimu ya Kiswahili, Ogisha Matale ni msanii wa kizazi kipya kutoka mji wa Goma,mkoani Kivu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wasanii katika kipindi hiki eneo lao likichukuliwa kuwa kitovu cha usalama mdogo. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.29/04/2023 20:42
-
Nyumba ya Sanaa Sagna: Msani wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Sagna ni miongoni mwa wasanii wachache kutoka kanda ya ziwa wanaofanya sanaa ya Muziki wa kizazi kipya, anapambana kufanikiwa licha ya changamoto. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.22/04/2023 20:02
-
Nyumba ya Sanaa Nyimbo za taarabu zinavyokubalika na mashabiki wa muziki huo: Rahma Machupa Naomba Stara ni miongoni mwa nyimbo za taarabu zinazokubalika na mashabiki wa muziki huo, katika eneo la Afrika mashariki na kati ambapo Rahma Machupa ndie muimbaji wa kibao hicho. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza nae huku ukipata vionjo vya muziki wake mtamu.08/04/2023 20:07
-
Nyumba ya Sanaa Vionjo vya muziki wa Bongo Fleva Makala ya Nyumba ya Sanaa ya juma hili inakuletea muziki wa Bongo Fleva ambao sasa unachagizwa na vionjo vipya, wasanii wachanga wanajiimarisha kwa kubobea na kutoa ladha inayokonga nyoyo za wapenzi waliokata tamaa, kutana na Zack Muziki akizungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.01/04/2023 20:04
-
Nyumba ya Sanaa SANAA NA ELIZABERT PASTORY KUHUSU USHAIRI Kwenye makala ya wiki hii Steven Mumbi amezungumza naye Elizabert Pastory kuhusu Ushairi.13/03/2023 20:01
-
13/03/2023 20:08
-
Nyumba ya Sanaa Sanaa ya Muziki na Zach Music Kwenye Makala ya wiki hii Steven Mumbi anazungumza naye Zach Music kuhusu masuala ya sanaa ya Muziki.13/03/2023 20:04
-
Nyumba ya Sanaa Sanaa ya Muziki wa kizazi kipya Kwenye Makala ya wiki hii ya nyumba ya sanaa, Mwandishi wetu Steven Mumbi anazungumzia kuhusu sanaa ya Muziki wa kizazi kipya.13/03/2023 20:11
-
Nyumba ya Sanaa Namna ya kuhifadhi ala na miziki ya kale nchini Kenya Ala za muziki zilizokuwa zinatumiwa zamani katika mataifa mengi ya Afrika, zimeanza kusahaulika. Huko nchini Kenya, serikali kupitia makavazi ya Bomas of Kenya, inahifadhi ala, muziki ,na tamaduni za kale/zamani kwa lengo la kudumisha , kuhifadhi na kufundisha utamaduni wa nchi hiyo. Mengi zaidi ni katika Makala haya, yanayomshirikisha Mwandishi wetu Steven Mumbi na Victor Abuso.04/06/2022 20:06
-
Nyumba ya Sanaa Muziki wa Abdulrazack Habibu kutoka nchini Tanzania Wiki hii mwandishi wetu Steven Mumbi anatoa nafasi kwa mwanamuziki Abdulrazack Habibu mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.19/03/2022 20:04
-
Nyumba ya Sanaa Maendeleo ya sanaa ya muziki wa injili nchini Tanzania Katika makala hii mwandishi wetu wa Daresalaam nchini Tanzania Steven Mumbi amejaribu kumdodosa mwanamuziki wa nyimbo za Injili maarufu sana nchini Tanzania Goodluck Gozbert kujieleza kuhusu juhudi za kukuza sanaa ya kuimba nyimbo za Injili, na mchango wao kama wanamuziki katika kufanikisha kuboreshwa maisha ya kikristo na kijamii kama ambavyo wanafanya viongozi wa kidini19/02/2022 20:05
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.