Visa vya wanawake na wasichana kubakwa nchini DRC
Imechapishwa:
Sauti 10:00
Wiki hii yameangazia vitendo vya ubakaji katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Shirika la MSF limesema katika mwaka mmoja uliopita ,limewatibu wahanga karibu elfu 11 wa ubakaji. Dhulma hizo zimechangiwa na utovu wa usalama ambao pia umeathiri utoaji huduma za matibabu ,huku mamlaka nchini humo zikishindwa kuwapa wahanga msaada wanaohitaji.