Siha Njema

Ugonjwa wa fistula waendelea kuwaathiri kina mama waliobakwa nchini DRC

Imechapishwa:

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wameendelea kuwahimiza wamama waliobakwa katika eneo lenye mizozo ya kivita huko mashariki ya nchi hiyo na baadaye kukumbwa na ugonjwa wa Fistula, kujitokeza katika kushiriki kampeini ya tiba bure. Miongoni mwa mashirika hayo ni pamoja na FISPRO lenye makao yake jijini Kinshasa na pia mjini Butembo, ambako inaarifiwa wamama hao bado wamekuwa wakijificha.  

Wamama waliotibiwa fistula kwenye mji wa Butembo, mashariki ya DRC Julai 2018
Wamama waliotibiwa fistula kwenye mji wa Butembo, mashariki ya DRC Julai 2018 © Ruben Lukumbuka/RFI Kiswahili