PAKISTAN-WAZIRISTAN

18 wauawa katika mashambulizi ya vikosi vya Marekani nchini Pakistan

Ndege ya Marekani isiyo na rubani inayotumiwa katika mashambulizi ya anga nchini Pakistan
Ndege ya Marekani isiyo na rubani inayotumiwa katika mashambulizi ya anga nchini Pakistan DR / RFI

Wapiganaji 18 wanaoshukiwa kuwa ni wa kundi la Al-Qaeda wameuawa nchini Pakistan kusini mwa mji wa waziristan kufuatia shambulio la bomu lililotekelezwa na vikosi vya marekani.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Pakistan katika mji huo amesema kuwa vikosi vya marekani vilifanya mashambulio matatu tofauti katika mpaka wa mji huo na nchi ya Afghanistan na kufanikiwa kuwaua watu hao 18.

Serikali ya Marekani hivi karibuni ilitangaza eneo hilo la Pakistan kama moja ya maeneo hatari zaidi duniani kwa kile ilichoeleza kuwa ndiko kuna ngome kubwa ya wafuasi wa Al-Qaeda pamoja na wanamgambo wapiganaji wa kundi la Taliban.

Mashambulizi hayo ya marekani yamefanyika mfululizo juma hili ambapo inaaminika kuwa katika mashambulizi ya siju ya Ijumaa mjini Waziristan mpakani mwa nchi hiyo na Afghanistan walifanikiwa kumuua kiongozi wa juu wa kundi la Al-Qaeda leney makazi yake nchini Pakistan Ilyas Kashmiri.

Shambulio hilo ambalo limeelezwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na vikosi vya marekani mwezi huu, limeteketeza kabisa ngome za wapiganaji hao, kuharibu nyumba pamoja na magari yaliyokuwa yakitumiwa na wapiganaji hao.

Tangu kuanza kwa mashmbulizi ya vikosi vya Marekani mwishoni mwa juma hili na kufanikiwa kuwateketeza wapiganaji hao wachambuzi wa masuala ya siasa wamekuwa wakihoji uimara wa vikosi vya Pakistan katika kukabiliana na wapiganaji hao.