UTURUKI-SYRIA

Idadi ya wakimbizi toka nchini Syria kuingia Uturuki yafikia 4,300

Baadhi ya wananchi wa Syria wakiwa na mabango yakipinga utawala wa Rais Bashar al-Asaad
Baadhi ya wananchi wa Syria wakiwa na mabango yakipinga utawala wa Rais Bashar al-Asaad Reuters

Wimbi la wakimbizi wanaoingia nchini uturuki kutokea nchini Syria limezidi kuongezeka ambapo maofisa wa Uturuki wanasema kuwa hizi sasa kuna zaidi ya wakimbizi 4300 ambao wameingia nchini humo kukimbia mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Maofisa nchini Syria wamesema kuwa wengi wa wakimbizi wanatokea katika mji wa Jisr el Shughor ambao umekuwa katika hali ya hatari tangu vikosi vya Syria vivamie mji huo kwa lengo la kuwasaka waandamanaji wanaotumia silaha kuwashambulia wanajeshi.
Siku ya ijumaa serikali ya Uturuki ilimtaka rais Bashar al-Asaad kuamuru vikosi vyake kuacha kufanya mashambulizi dhidi ya waandamanji kwa kile ilichoeleza kuwa kuendelea kuwashambulia wananchi kunaongeza wimbi la wakimbizi kuingia nchini humo.

Viongozi hao pia wameonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka maradufu kwakuwa kuna taarifa kuwa bado vikosi vya Syria vinaendelea na operesheni zake za kuwasmabaratisha wapiganaji wenye silaha.

Kwa upende wake serikali Syria imeendelea kupuuza onyo la umoja wa mataifa na nchi ya Uturuki wa kuitaka nchi hiyo kusimamia amani na kuacha kukiuka misingi ya haki za binadamu ambayo mpaka sasa inafanya wananchi kuikimbia nchi yao.

Rasi Asaad mwenye ameendelea kusisitiza kuwa vikosi vyake vitaendelea na operesehni mjini Jisr na vitongoji vyake hatua inayoonekana kulipiza kisasi tangu kuuawa kwa maofisa 120 wa jeshi lake.