INDIA-MUMBAI

Mtuhumiwa wa mabomu mjini Mumbai, India akata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo aliyopewa

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya mabomu mjini Mumbai nchini India mwaka 2008 amewasilisha rufaa yake katika mahakama kuu ya nchi hiyo akipinga adhabu ya hukumu ya kifo aliyopewa.

Mohammad Ajmal Amir Qasab, mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Mumbai, India
Mohammad Ajmal Amir Qasab, mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Mumbai, India Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mtuhumiwa huyo Mohammad Ajmal Amir Qasab ambaye ndiye mtuhumiwa pekee aliyenusurika na kukamatwa katika mashambulizi hayo amewasilisha rufaa yake kupitia mkuu wa gereza ambalo anashikiliwa.

Mwendesha mashtaka Ujjwal Nikam amedhibitisha mtuhumiwa huyo kuwasilisha rufaa yake katika mahakama kuu nchini humo akipinga huku ya kifo aliyopewa ambapo mahakama inapanga tarehe ya kusikiliza shauri hilo.

Hii inakuwa rufaa ya pili kukatwa na mtuhumiwa huyo ambapo mahakama hiyo ilitupilia mbali rufaa yake mwezi wa pili mwaka huu na kumtaka kuiandika upya ambapo sasa inasubiriwa kutoa uamuzi kuhusiana na rufaa yake.

Tukio hilo ambalo lilishuhudia watu zaidi ya 50 wakipoteza maisha lilisababisha kutokea mtafaruku wa uhusiano kati ya nchi za India na Pakistan kwa nchi ya India kuishutumu Pakistan kufadhili vikundi vya kigaidi.

Mohammad Ajmal Amir Qasab alihukumiwa kunyongwa mwezi wa tano mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki na kupanga mashambulizi hayo.