Yemen

Serikali ya Yemeni yathibitisha kifo cha kiongozi wa Al Qaeda

RFI

Wizara ya ulinzi ya nchini Yemen imethibitisha kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Anwar Al Awlaki na wapiganaji kadhaa siku ya ijumaa alfajiri katika shambulio la ndege lililotekelezwa katika jimbo la Marib ambalo linaaminika kuwa ngome kubwa ya kundi la al qaeda magharibi mwa yemen.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ulinzi ya nchini Yemen imetoa taarifa za kutokea kwa vifo hivyo na kushindwa kufafanua mazingira ya vifo hivyo.

Maafisa wa marekani ambao hawakutaja majina yao wamesema kuwa kiongozi huyo wa al qaeda ameuawa na majeshi ya marekani katika shambulio la anga lililotekelezwa mashariki mwa jimbo la Marib eneo linalosadikiwa kuwa ngome ya al qaeda.

Maafisa hao wamethibitisha kuwa ndege za kijeshi za marekani zimekuwa zikifanya mawindo katika jimbo la marib kwa kipindi cha siku kadhaa ambapo raisi wa marekani Barack Obama alitoa agizo la kuuawa kwa kiongozi huyo.

Taarifa za vifo hivyo zinaamsha wasiwasi jijini Washngton kufuatia madhara ya mgogoro wa kisiasa nchini Yemen kutishia kudhoofisha jitihada za kupambana na majeshi ya kundi la Al Qaeda.