Syria

Wapinzani wa Syria wanakutana kupinga ukandamizaji na upotevu wa maisha ya wanadamu nchini humo

Wawakilishi wa waandamanaji wa nchini Syria wameunda umoja wa upinzani huko nchini Uturuki hii leo kwa ajili ya kuweka nguvu ya pamoja dhidi ya utawala wa rais wa Syria Bashar Al Assad .Mjini Instambul baraza la taifa la Syria linalofanya juhudi za kuunganisha vyama vya upinzani vya Syria limefungua mkutano wa siku mbili kwa ajili ya kuteua uongozi wa upinzani.

WAnanchi wa Syria wakiandamana tarehe 16/9/11.
WAnanchi wa Syria wakiandamana tarehe 16/9/11. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, hii leo raia watano na wanajeshi na wanausalama sita wameuawa katika kijiji cha Kafar Zita, Ofisi ya tume ya umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya haki za binaadam imesema idadi ya waliopoteza maisha kutokana na machafuko ya nchini humo imefikia zaidi ya 2700 tangu tarehe 15 mwezi march.