Yemeni

Watu zaidi waendelea kuawa nchini Yemen katika shinikozo la kumtaka rais aachie ngazi

Maandamano jijini Sanaa ya kumtaka rais Ali Abdallah Saleh aachie madaraka, Jumapili Octoba 16, 2011.
Maandamano jijini Sanaa ya kumtaka rais Ali Abdallah Saleh aachie madaraka, Jumapili Octoba 16, 2011. REUTERS/Khaled Abdullah

Watu kumi na mbili wamekufa wakiwemo wanajeshi saba kufuatia vurugu zilizozuka wakati polisi walipokuwa wakikabiliana na maelfu ya waandamanji katika mji mkuu wa Yemen Sanaa wakishinikiza kujiuzulu kwa rais Ali Abdulah Saleh.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na wanaharakati nchini humo imedhibitisha kuuawa kwa waandamanji saba wakiwemo polisi na kuongeza kuwa wanajeshi wa serikali wamekuwa wakitumia risasi za moto kuwashambulia waandamanaji na kusababisha vifo hivyo.

Maandamano hayo yameitishwa nchi nzima kushinikiza kujiuzulu kwa rais Saleh pamoja na kulitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UN kuingilia kati mgogoro huo huku waandamanji hao wakiapa kufanya maandamano hayo kwa siku kumi mfululizo mpaka utawala wa rais Saleh utakapong'atuka.