Palestina

Wazazi wa Shalit walipoteza matumaini ya kumuuona tena

Mwanajeshi wa Israeli ambaye alitekwa kwa kipindi cha miaka mitano na Kundi la Wanamgambo la Hamas lililopo nchini Palestina Gilad Shalit hatimaye amewasili nchini mwake huku kundi la wafungwa 477 nao wakitua Palestina.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shangwe ndiyo ambayo imetanda katika pande mbili hasimu yaani Israeli na Palestina na kwa sasa tofauti zao ni kama vile zimewekwa kando baada ya kufikiwa makubaliano ya kubadilishana watu ambao walikuwa wanashikiliwa na kila upande.

Mwanajeshi Shalit aliwasili nchini Israel na kupokelewa kama mfalme huku wafungwa wa Palestina nao wakipata mapokezi makubwa zaidi wakiendelea kusubiria kundi jingine ambalo limesalia kuachiwa.

Baba Mzazi wa Shalit, Noam Shalit amewaambia wanahabari kwa mara nyingine anaona kama mtoto wake amezaliwa upya kwani hawakuwa na matumaini ya kumuona akirejea hai nchini Israeli.

Muafaka baina ya Israeli na Palestina ulifikiwa mwishoni mwa juma lililopita ambapo Israel ilitakiwa uwaachie wafungwa 1,021 ili iweze kupatiwa mwanajeshi wake Shalit ambaye alikamatwa miaka mitano iliyopita ambapo wenzake wawili walipigwa risasi.