SYRIA-DAMASCUS

Rais wa Syria ayaonya mataifa ya magharibi dhidi ya kuchochea vurugu nchini mwake

Rais wa Syria Bashar Al Assad ameionya maafa zaidi yatashuhudiwa nchini mwake iwapo mataifa ya Magharibi yataingilia wakati huu ambapo Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ikianzisha juhudi za kudhibiti umwagaji wa damu unaoshuhudiwa kwenye taifa hilo. 

Wananchi wa Syria wakiandamana
Wananchi wa Syria wakiandamana REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

waziri wa mambo ya nje wa Qatar,sheikh hamad bin Jassem amesema mawaziri kutoka umoja huo wamekubaliana kuja na mapendekezo ya kukomesha aina zote za ukandamizaji na nchini Syria.

Baada ya onyo la rais Assad juu ya kutoingiliwa na mataifa ya magharibi,sheikh Hamad amesema jhali itakuwa mbaya zaidi ikiwa Damascus haitachukua hatua madhubuti kukomesha machafuko nchini Syria.

Hamad amesema kuwa hivi sasa Syria haina budi kuchukua hatua hiyo ili kuepuka yale yaliyotokea katika mataifa mengine ya kiarabu hasa nchini Libya hususan baada ya majeshi ya NATO kuingilia kati.

Ujumbe wa Syria utaendelea kubaki mjini Doha nchini Qatar ili kutoa majibu ya Assad baada ya mapendekezo kutolewa na umoja huo.